Mbunge Chadema Akerwa Uhamiaji Kuhoji Uraia Wa Askofu - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Tuesday, 12 December 2017

Mbunge Chadema Akerwa Uhamiaji Kuhoji Uraia Wa Askofu


Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amekerwa na madai ya taarifa za kuhojiwa kwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenga, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi (61) na Idara ya Uhamiaji kuhusu uraia wake. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Heche amesema utawala wa Kikwete Kanisa lilisimama imara kukosoa mambo kadhaa wakati ya Serikali na hakuwahi kushuhudia viongozi wa dini wakihojiwa. Amesema Askofu Niwemugizi ameohojiwa kwa kuwa alisema imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira nzuri ambayo pia italetwa na Katiba Mpya na kusisitiza kwamba. “Kanisa lilisimama imara kukosoa mambo kadhaa wakati wa utawala wa Kikwete, sikuona kiongozi anahojiwa uraia wake naamini ingekuwa kipindi hiki kanisa lingefutwa wangesema sio kanisa la Kitanzania, tusimame imara kupinga uhuru wetu
kuporwa, hakuna alie salama” Heche . Inadaiwa kuwa Askofu Niwemugizi alihojiwa mara 2 na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na Uraia wake kati ya mwezi Novemba na Disemba

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.