Mbunge wa Iringa Mjini CHADEMA, Peter Msigwa.
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi hivi karibuni wamekuwa wakisema upinzani Tanzania unakufa kwa vile hawana ajenda zenye mashiko kwa sasa hivyo kupelekea baadhi ya wanachama wao kuhamia chama cha Mapinduzi (CCM). Kutokana na Kauli hiyo Mbunge wa Iringa Mjini CHADEMA, Peter Msigwa amehoji kuwa endapo upinzani ukifa je ndiyo maendeleo ya nchi yatapatikana?. “Mkutano wa UVCCM ulibebwa na kibwagizo cha upinzani kuwa unakufa! Fine, tukubaliane kuwa upinzani unakufa! Ukifa upinzani zitaongezeka ajira ngapi! Umaskini utapungua kwa kiwango gani? Haki za binadamu zitalindwa kwa kiwango gani? Utawala bora utaimarika kwa kiwango gani ? Demokrasia itaimarishwa kwa kiwango gani? Uhuru wa kutoa mawazo na vyombo vya habari utaimarika kwa kiwango gani! Haya yote hayana chama! Nilitegemea CCM mje na majibu ya haya sio upinzani unakufa” Amesema Msigwa Hoja upinzani unakufa imeendelea kushikiwa bango na makada wa CCM wakidai kuwa vyama vya Upinzani vimekua havina ajenda kwa sasa kwa sababu baadhi ya vitu walivyokuwa ndio ajenda yao ndivyo vinatekelezwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.