Mbowe kusaka dhamana kesho Mahakama Kuu - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Tuesday, 5 March 2019

Mbowe kusaka dhamana kesho Mahakama Kuu






MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuendelea na usikilizwaji  wa rufaa ya Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini
arehe mosi Machi wiki iliyopita Mbowe na Matiko waliruka kiunzi cha waendesha mashataka baada ya Mahakama ya Rufaa kuitupilia mbali rufaa ya serikali iliyolenga kukwamisha usikilizwaji wa  rufaa ya dhamana kwenye mahakama hiyo.
Mkurugenzi wa Mashtaka DPP alikata rufaa hiyo kupinga usikilizwaji wa dhamana hiyo kwa madai kuwa Mahakama Kuu haikuwa haki kamili ya usikilizwaji.
Aidha, Majaji wa Mahakama ya Rufaa walieeleza kuwa DDP alikosea kuwasilisha shauri hilo mahakamani hapo, wakati shauri la msingi bado linaendelea Mahakama Kuu.
Katika shauri hili, DDP iliwasilisha hoja mbili za kuomba rufaa Na. 344 iliyopo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, iondolewe mahakani hapo.
Shauri hilo lilisiikilizwa na jopo la majaji watatu – Gerald Ndika, Stella Mgasha na Mwanaisha Kwaliko.
Mbowe na Matiko, kupitia mawakili wao, Peter Kibatara na Prof. Abdallah Safari, waliwasilisha Mahakama Kuu, maombi ya kurejeshewa dhamana yao, kufuatia kufutiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, tarehe 30 Novemba 2018.
Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri, kwa alichokieleza kuwa wamekiuka masharti ya dhamana.
Hoja za upande wa serikali juu ya rufaa hiyo, ni pamoja na Mahakama Kuu kutotoa muda wa kuwasikiliza wakati wa usikilizwaji wa rufaa ya Mbowe na Matiko.
Katika shauri hilo la jinai, DPP aliwasilishwa na wanasheria wake wawili, Faraja Nchimbi na Paul Kadushi.
Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai, mkoani Kilimanjaro na Matiko, walifutiwa dhama zao tarehe 23 Novemba 2018, kufuatia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kudai kuwa imejiridhisha kwamba wote wawili, walitenda kinyume na masharti ya dhamana walizopewa.
Katika kesi ya msingi, Mbowe, Matiko na watu wengine saba, wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai. Wanadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya 1 Februari na 16 Machi, mwaka jana, maeneo ya Dar es Salaam.
Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo, ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji; Mbunge wa Iriga Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Kibamba na Katibu wa Chadema, Tanzania Bara, John Mnyika.
Wengine, ni Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho (BAWACHA), Halima Mdee; Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.