MBUNGE ADAI POLISI WALIMTESA - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Tuesday, 12 December 2017

MBUNGE ADAI POLISI WALIMTESA



Image result for Pauline Gekul

MBUNGE ADAI POLISI WALIMTESA
Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul (Chadema) amesimulia jinsi alivyokamatwa na polisi akiwa na mawakala katika uchaguzi mdogo wa udiwani Novemba 26.
Alisema yeye hakutekwa bali alichukuliwa na polisi kwenda kituo cha polisi, Usa River baada ya kuhojiwa sababu za mawakala wa Chadema kuondolewa kwenye vituo. Gekul alisema kuwa msimamizi wa kata ya Reguruki wilayani Arumeru ambayo ilikuwa inafanya uchaguzi wa diwani .
Alidai kuwa kilichofanyika ni uhuni na ukiukwaji mkubwa wa demokrasia .
“Kwa kweli kwa yale yaliyofanyika Arumeru hakuna demokrasia tena Tanzania.
“Ikibidi Rais alete muswada bungeni tufute mfumo wa vyama vingi uliopo,” alisema Gekul na kuongeza:
“Mfano mtu wa kwanza alipokuwa anaingia kituo cha kupigia kura kama pale Reguruki alikuta sanduku la kura limeishafika nusu na alipouliza aliambiwa atoke nje wakati alikuwa hajawekewa hata mhuri kiganjani.”
Mbinge huyo alisema siku ya uchaguzi wananchi walipata hofu kwamba mbunge wao alitekwa baada ya kuona anachukuliwa na polisi. Alisema mmoja wa mawakala aliyekamatwa naye alipata mshtuko na kutapika kabla ya kupelekwa kituo cha afya na kupatiwa matibabu.
Mwanasiasa huyo alisema kilichofanyika Arumeru ni ubakaji wa demokrasia kwa sababu mawakala wote walikuwa na barua kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na waliapishwa na watendaji wa kata.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.