Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amekosoa msamaha wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa familia ya Babu Seya, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanae Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa ubakaji wa watoto. Zitto ametoa ya moyoni kupitia ‘post’ mbalimbali ambazo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya kijamii tangu kutangazwa kwa msamaha huo jana ambapo Rais Magufuli alitoa misamaha kwa zaidi ya wafungwa 8,000 na wengine 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa. Kwa mujibu wa Zitto, amebainisha kuwa wabakaji hawapaswi kusamehewa kiholela.
Hatahivyo, Rais Magufuli alifanya hivyo kulingana na Ibara ya 45 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwezesha Babu Seya na Papii Kocha kuwa nje ya gereza jana jioni ambapo mara tu baada ya kutoka wawili hao wakiwa na magitaa yao mgongoni walielekea katika Kanisa la Life Christian, lililopo Tabata Segerea, Dar es Salaam, kukutana na Mchungaji. “I have read judgement that convicted Babu Seya and son. And judgements at the high court appeal, appeal at court of appeal and petition at African Court. I am appalled by decision to pardon convicted rapists. Devastated by statements to congratulate such a decision” ZZk. “Waliozomea na kuzodoa ahadi ile walikuwa sahihi. Wanaomzomea Rais kwa kutoa msamaha wapo sahihi pia. Hakuna sababu kuzodoana. Tukemee wabakaji kusamehewa kiholela” ZZK.,” ameandika Zitto.
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.