Dodoma. Serikali imesema shule za
taasisi za dini zimepoteza mwelekeo kwa kuwa zimeanza kuzalisha vijana wa
vijiweni na baadhi zinatajwa katika suala la ushoga.
Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa
na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Maria
Semakafu wakati akifungua mkutano wa umoja wa shule za seminari na binafsi
uliofanyika mjini hapa.
Dk Semakafu alikemea tabia ya ushoga kuwa imeanza kuota mizizi kwani vijana wengi wa mitaani wakiulizwa mambo ya ushoga walijifunzia wapi wanazitaja shule za dini.
"Haya siyo maadili mliyokuwa mkifundisha tangu awali, kafundishe maadili ya kidini kama mlivyokuwa awali, tunapata malalamiko mengi kutoka kwa wazazi na wanafunzi wanaosoma huko kuhusu tabia hizo chafu," amesema Semakafu.
Amesema kwa sasa shule hizo zimekuwa na maadili mabovu akaagiza warekebisha mienendo yao haraka kwani Serikali haitavumilia vitendo hivyo.

No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.