
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Sadifa Juma Khamis (MB) amekamatwa na Maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) nyumbani kwake eneo la Mnada wa Zamani, Dodoma akigawa rushwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM Taifa toka mkoa wa Kagera kwa ajili ya mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho.
Hivi sasa yupo Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma...
UPDATES:
08:30pm - December 09, 2017
Taarifa ambazo zimethibitishwa na JamiiForums, zimebainisha kuwa Sadifa amekamatwa kweli na pesa hizo inadaiwa zilikuwa za mgombea mmojawapo anayeitwa “Thobias” ambaye anadaiwa alimpa Mwenyekiti huyo awape wajumbe.
11:00am - December 10, 2017
- Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Emma Kuhanga amethibitisha kukamatwa kwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Khamis kwa tuhuma za kugawa rushwa
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.