
WARAKA WA
MBUNGE WA ARUSHA MJINI KWENDA KWA RAIS. kabla hujasoma share ufike ikulu.
Godbless J Lema
Arusha MP
✅
#1 Today at 7:59 AM
New
Mh. Rais nakusalimu.
Arusha MP
#1 Today at 7:59 AM
New
Mh. Rais nakusalimu.
Uchaguzi wa
marudio viti vya udiwani umekwisha, tumeshuudia nguvu ya dola kwa dhati kabisa
nimeona kila kitu kilichotokea na bado siamini kama ni Tanzania kwa uchaguzi wa
aina hii.
Mh. Rais,
kuibiwa kura ni tofauti na kuporwa ushindi, huku kwetu Arusha huu sio wizi wa
kura huu ni unyang,anyi wa kura, watu wameona na kushuudia ukatili wa ajabu wa
Polisi na wasimamizi katika uchaguzi huu kwa kweli nimeumia sana kuliko wakati
wote wa maisha yangu kwani ninatafakari ni wapi Nchi yangu inakwenda? Kwa namna
hii wasiwasi mkubwa nilio nao ni maamuzi ya watu katika mioyo yao sioni kana
kwamba watu hawa watalia tu bila kutafakari hatima yao, kwa namna nilivyoona ni
dhahiri niseme kuwa Tanzania hakuna tena uchaguzi.
Matendo haya
ya kwenye uchaguzi huu wa jana yameharibu fikra za watu wengi juu ya hatima ya
Nchi yao na uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama vimetekeleza wajibu huu wa
uporaji ushindi kwa nguvu zote. Kwa mfano, huko Meru na katika kata ya Muriet,
wakala aliyekataa kutoka nje wakati wa zoezi la kuhesabu kura, kwa kweli
alipata shida sana, wakala wetu kijana mdogo Edwin alipigwa vibaya na
wasimamizi wa Tume alipokataa kutoka nje ya kituo cha kura baada ya
kulazimishwa kutoka nje. Lakini pia nilishuhudia kwa macho yangu wakala wetu
kijana Nuhu akitolewa kwenye kituo na askari kwa nguvu na kudhalilishwa sana,
nilitamani nishuke nimsaidie lakini niliingiwa hofu kwani nilikuwa na taarifa
mbaya zilizopangwa juu ya maisha yangu.
Mh. Rais,
hekima inalia sana, mioyo ya watu wote walioshuhudia huu uchaguzi ni maoni yangu
kuwa sasa bila shaka wanatafakari namna nyingine ya kupata viongozi wao, kwa
vile ni dhahiri kuwa Uchaguzi hauna uhakika ya kutoa nafasi ya watu kuamua. Je,
unafikiri ni nini itakuwa hatma ya Tanzania baadae?
Mh. Rais,
kama huu ni mkakati wa kumaliza Upinzani, pengine mkakati huu unaweza
kufanikiwa, lakini Nchi haiwezi kuwa salama hata kidogo. Hapa ndipo napata
mashaka hivi kweli mtoto wangu na wajukuu zako wataishi vipi katika Taifa kama
hili? Ni uhakika kwamba Polisi na hata Tume waliofanikisha zoezi hili miongoni
mwao baada ya jana watakuwa miongoni mwa watu ambao wanatafakari sana kuhusu
hatima ya Nchi yao.
Mh. Rais,
CCM kushangilia ushindi huu ni fedheha na kejeli kubwa kwa Mungu, lakini kwa
vile tulifundishwa tukiwa wadogo kuwa Mungu anaishi mbinguni basi bila shaka
Mungu atakuwa anaanda safari ya kuja huku kwetu Tanzania hivi karibuni.
Uchaguzi huu umeongeza chuki na uadui mkubwa sana miongoni mwa jamii. Mtu
anawezaje kusema anaipenda Nchi yake na kuacha mambo kama haya yatokee?
Mh. Rais,
nimekusikia mara nyingi ukimtaja Mungu kinywani mwako, kama kweli ni huyu Mungu
wa kweli aliye umba mbingu na Nchi ni sahihi nikisema huyu Mungu hawezi
kuruhusu wala kuvumilia mambo kama haya yafanyike. Watu wamepigwa, wamekatwa
mapanga na fedhea mbali mbali, hakika damu itanena tu.
Mh. Rais,
ninakuomba kuchukua tahadhari sana na watu wanaosema kila kitu ndio mzee, hawa
ni maadui zako na Nchi yako. Huko Zimbabwe pia walikuwepo kwa Mugabe, lakini
tumeshuhudia Watu wale wale walivyokuwa wa kwanza kusema Mugabe asulubiwe.
Mh. Rais,
ninao uhakika kwamba kila jambo lina wakati wake, ni busara kila nyakati
ikatumiwa kwa busara, kwani nyakati ni mbegu na maandiko yanasema “Mungu
hadhihakiwi, apandacho Mtu ndicho avunacho”. Sasa uchaguzi huu umekwisha kwa
namna hii watu wote wakiwemo vyombo vya ulinzi na usalama waliioshiriki ktk
uchaguzi huu waeona ukatili mkubwa dhidi ya haki na maamuzi ya watu katika
chaguzi.
Mh. Rais,
nimalizie kwa kusisitiza kuwa, hiki kilichotokea katika uchaguzi huu wa marudio
ni hatari kwa usalama wa Nchi, sitatajii kuamini kwamba nitaeleweka kwa ujumbe
huu, sasa mpango wa kuondoa kwenye nafasi zao viongozi mbali mbali Nchini
utaendelea kwa namna na njia yoyoye ile kwani wana uhakika kuwa wakirudi kwenye
uchaguzi watatangazwa washindi.
Mh. Rais,
hatuwezi kuvunjika moyo hata kidogo na siku zote tunaimarika kutokana na
matatizo na changamoto, tunayo fursa sasa ya kufikiri kwa dhati ni nini hatima
ya Tanzania na uchaguzi. Bila shaka sasa wananchi tutaanza kudai Katiba huru
kwa nguvu zote na haya ndio madai yetu ya msingi kwa wakati huu kuliko jambo
lolote, najua sasa Watanzania watakuwa tiyari, bila Katiba na Tume huru
Tanzania hakuna Tume ya uchaguzi bali kuna tume ya uporaji wa uchaguzi.
Mh. Rais,
tafadhali naomba utafakari maneno haya aliyosema mfalme Sulemani kutoka katika
kitabu cha Mithali. "Kabla ya uharibifu
moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu"
Mungu
akubariki sana.
ONLY TIME WILL TELL.
ONLY TIME WILL TELL.
Godbless J Lema (MB)
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.