Mbunge
wa Mtama, Nape Nnauye, amekiri kuwepo na vitendo ambavyo siyo sahihi ambavyo
vilivyojitokeza katika Uchaguzi
wa
marudio katika baadhi ya kata na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe.
Nape
amefafanua hayo baada ya kuwepo na malalamiko hayo kutoka upande wa
upinzani ambapo amesema kwamba vitendo hivyo vinapaswa kushughulikiwa
kisheria kama wahalifu na siyo kushughulikiwa kisiasa na kwamba kufanya
matendo hayo kisiasa ni njia za kuficha uovu.
Pamoja
na hayo Nape ameongeza kwamba hajawahi kuwa muumini wa matumizi ya nguvu kwenye
siasa na wala hajawahi kushiriki mipango ya kutumia nguvu bali anaamini katika
matumizi zaidi ya nguvu.
Aidha
Nape ameongeza kwamba sehemu zote alizofanya kampeni na wala hakubariki
matumizi ya nguvu hivyo kuwashauri vyama vya upinzani wafanye tathmini ya kweli
kisha kuchukua hatua pale walipoteleza katika uchaguzi.
"Rafiki zangu
Upinzani fanyeni tathmini ya kweli halafu chukueni hatua pale mlipoteleza.
Hichi kinachoendelea cha kutoa visingizio vya jumla. Sikatai kuwa kulikuwa na
baadhi ya maeneo kumekuwa na vitendo si vya kibinadamu lakini si kwa kata
zote. Vitendo hivyo vishughulikiwe specific kisheria kama wahalifu na si
kushughulikiwa kisiasa".Amesema
Nape
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.