WAKATI Uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika jana
nchi nzima kutajwa kugubikwa kwa vitendo vya utekaji
kwa wabunge
wa Upinzani,pamoja na kufukuzwa kwa mawakala
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kwenye vituo vya kupiga kura, Hali hiyo imemubia
Mbunge wa jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CMM Mh.
Ridhiwani Kikwete baada ya kueleza kutofurahishwa na
vitendo vya uvunjivu wa amani na migawanyiko,
vilivyojitokeza katika uchaguzi huo mdogo ambao
Chadema walisusika kata tano
Aidha Ridhiwani ametoa ushauri
unaolenga kuondoa visingizio na propaganda za kutumia wanachama kama ndio
sehemu ya vurugu hizo akidai kuwa wafanya vurugu hao ni wananchi na sio CCM
wala CHADEMA kama ambavyo kila upande unadai.
“Wanaopigana ni wananchi,
sio CCM wala CHADEMA, maana naona pande zote zinalalamika, tuwe na hukumu
sahihi, la msingi tukatae fujo, nchi hii ni muhimu na tuenzi mawazo sahihi ya
wazee wetu”, ameongeza Ridhiwani.
Wananchi katika Kata 43 za
mikoa 19 nchini kote jana wamepiga kura kuchagua madiwani katika uchaguzi mdogo
ambapo vitendo kadhaa vya vurugu viliripotiwa kutokea huku CHADEMA ikijitoa
kushiriki uchaguzi huo katika kata 5 za wilaya ya Arumeru
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.