RC MAKONDA AZUIA TAMASHA LA FIESTA KUFANYIKA DAR ES SALAAM - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Saturday, 18 November 2017

RC MAKONDA AZUIA TAMASHA LA FIESTA KUFANYIKA DAR ES SALAAM

Image may contain: 1 person, sitting and close-up
Zikiwa zimebakia siku chache kabla ya kufanyika kwa tamasha la Fiesta, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda amepiga marufuku matamasha yoyote ya muziki yanayozidi saa 6 usiku. Makonda amesema muda wa matamasha ya nje ni saa 6 usiku, na yeyote atakayezidisha muda huo atachukuliwa hatua kali kwa kuvunja sheria.
_
"Bado sheria haijabadilika. Mwisho wa matamasha ya muziki ya nje na kwenye bar ni saa 6 usiku. Anayetaka kuendelea aende club." Amesema Makonda leo kupitia Efm na kusisitiza kuwa amewaagiza Polisi kuzuia tamasha lolote litakalozidi saa 6 usiku, na kusema yeye mwenyewe huwa anatembea usiku kwahiyo atafanya monitoring kuhakikisha hakuna tamasha litakaloendelea baada ya muda huo.
Nini maoni yako??

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.