MADHARA YA RUSHWA KWA MAENDELEO YA AFRICA - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Sunday, 5 November 2017

MADHARA YA RUSHWA KWA MAENDELEO YA AFRICA


The picture was used to illustrate the level of corruption in Ukraine in the year 2016.

MADHARA YA RUSHWA KWA MAENDELEO YA AFRICA

Rushwa ipo kila mahali na asili ya rushwa inategemea na mazingira ya eneo husika.rushwa imegawanyika katika vipengele tofauti na inategemeana Mtoaji wa Rushwa na Mpokeaji  wa Rushwa wapo katika mazingira gani.
Bara la afrika kwa asilimia 80% linakaliw na watu weusi(black race), Bara la Afrika lina rasimali mbali mbali ambazo bado hazijafanyiwa ufumbuzi wa kutosha namna gani ya kuzitumia ili zitumike kuleta kipato na kusaidia maendeleo kwenye bara husika, Baadhi ya rasimali za Afrika ni kama zifuatazo, MADINI, Afrika ina utajiri wa kuwa na madini mbalimbali kama gold, diamond,tanzanite,rubies, copper na aina zingine  za madini,GESI YA ASILI, VIVUTIO VYA ASILI, lakini bado Africa inaonesha kuwa kinara wa rushwa Tafiti zilizofanywa na Taasisi zinahusika na rushwa Duniani zinaonesha Afrika imekithiri kwa  vitendo vya rushwa.
Vitendo vya rushwa vimelifanya bara la Afrika kuonekana bara la ovyo kabisa na kuwa nyuma kimaendeleo.
Kwa mfano kwenye Nchi za Afrika unaweza kuwalipa /kumlipa polisi au Afia wa polisi ili akufichie makosa yako. Asilimia 75% watu hutoa rushwa ili kuepuka adhabu ya polisi au ya mahakama na wengine wametoa rushwa ili kupata huduma za msingi , na wengine wametoa rushwa ili kupata kazi
Askari wa usalama barabarani akipokea Rushwa.

JE RUSHWA HUSABABISHWA NA NINI
Barani Afrika rushwa inasababishwa na vitu vingi kama-:
          Utawala mbovu/ mbaya
          Tamaa
          Kutokuwajibika kwa viongozi na Taasisi
          Ukosefu wa Ajira
          Tamaa ya kutajirika mapema
MADHARA YA RUSHWA KWENYE BARA LA AFRIKA
Kudidimia kwa maendeleo
Umaskini wa kukithiri
Ukosefu wa ajira
Kudidimia kwa huduma za jamii
Vita vya wenyewe kwa wenyewe
Kushuka kwa ubora wa Elimu




         


No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.