UTEUZI WA DK SLAA KUWA BALOZI WAMUIBUA PROFESA LIPUMBA,SOMA HAPO KUJUA
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama
cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
amezungumzia uteuzi wa Dk Wilbroad Slaa
kuwa balozi akisema hakutarajia.
Rais John Magufuli juzi alimteua Dk Slaa
aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Chadema
kabla ya kukihama chama hicho wakati wa
kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Wakati wa mchakato wa uchaguzi huo,
Profesa Lipumba na Dk Slaa ambao vyama
vyao vilikuwa katika umoja uliojulikana
Ukawa, walijiondoa baada ya Chadema
kumpitisha Waziri Mkuu wa zamani
Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa
urais.
Akizungumza na Mwananchi jana, Profesa
Lipumba alisema, “Imekuwa kama surprise,
sikutegemea kama Dk Slaa atateuliwa kwa
sababu muda mwingi yupo Canada.”
Hata hivyo, Profesa Lipumba alisema hana
shaka na uteuzi huo kwa kuwa Dk Slaa nimzoefu wa siasa na mzalendo ambaye
ataitumikia vyema nafasi hiyo mpya.
“Narudia, sikutegemea. Ila popote
atakapopangiwa kazi Dk Slaa atafanya kwa
sababu najua ni mchapakazi,” alisema.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
alisema Rais Magufuli ana mamlaka
kisheria ya kumteua mtu atakayemuona
anafaa katika nafasi fulani.
“Huu ni uamuzi wa Rais sisi wengine hatuna
comments zaidi ya kuwatakia kila heri
katika utendaji wao wa kazi,” alisema
Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai mkoa
wa Kilimanjaro.
Akizungumza uteuzi huo wa Dk Slaa, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa
Abdallah Safari alisema Rais Magufuli
amemuonea huruma Dk Slaa ndiyo maana
akaamua kumpa nafasi ya ubalozi.
Profesa Safari alisema hawezi kumsema
vibaya Dk Slaa lakini nafasi hiyo ni huruma
na zawadi ya Rais Magufuli.
Amedai Dk Slaa alijaribu kuivuruga
Chadema wakati wa uchaguzi mkuu mwaka
2015 lakini hakufanikiwa.
“ Hii ni huruma. Siku zilizopita Dk Slaa
aliandikwa katika vyombo vya habari kuwa
anafanya kazi Super Market. Mimi nimekaa
Ulaya najua maisha ya kule na Dk Slaa ni
rafiki yangu sana lakini kwa kitendo
alichokifanya mwaka juzi, haya ndiyo
matokeo yake,” alisema Profesa Safari.
Kwa upande wake, aliyewahi kuwa Balozi
wa Tanzania nchini Urusi kuanzia mwaka
2002 hadi 2008, Patrick Chokala
alimpongeza Rais Magufuli kwa kumteua
Dk Slaa kuwa balozi.
“Sina shaka hata kidogo na Dk Slaa ana
uwezo wa kufanya kazi nchi yoyote. Hii kazi
anaiweza na ni mtu mwenye dhamira ya
kweli,” alisema Balozi Chokala.
Alisema anamfahamu Dk Slaa kwa kipindi
kirefu tangu akiwa padre na kwamba,
amekuwa ni mchapakazi hodari na mwenye
hekima kwa watu.
Akizungumza na kituo cha televisheni cha
Azam TV, Dk Slaa alimshukuru Rais
Magufuli kwa kumteua ili aungane nayekujenga nchi na hivyo atafanya kazi kwa
uwezo wake wote.
Dk Slaa ambaye hivi sasa anaishi Canada
alisema, “Ni mapenzi ya Mungu, nashukuru
kwa uteuzi. Ninachoweza kusema katika
hatua hii, huu ni wajibu mkubwa kwenye
kipindi cha kulijenga Taifa letu
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.