GENGE linalojitambulisha kuwa linamwakilisha Profesa Ibrahim Lipumba katika kinachodhihirika kuwa na lengo la kukidhoofisha Chama cha Wananchi (CUF) likiwa limekwama kupata ruzuku, sasa limeamua kumtaka jaji ajitoe, anaandika Faki Sosi. Hali hii imejionesha pale mawakili wa upande huo wakiongozwa na Mashaka Ngole, walipowasilisha mbele ya Mahakama Kuu, hoja ya kutaka Jaji Wilfred Dyansobera ajitoe katika usikilizaji wa kesi zilizofunguliwa wakati chama hicho kikikabiliwa na mgogoro mkubwa kiuongozi. Wakili Ngole alitoa hoja kwamba Jaji Dyansobera asisikilize kesi hizo na badala yake jukumu hilo apewe Jaji Suleiman Kihiyo ambaye ndiye alianza kusikiliza kesi hizo katika hatua za mwanzo za ufungiliwaji wa kesi, kabla ya mawakili wa CUF kumtaka ajitoe.
Hoja hiyo ilikuja mahakamani tarehe 31 Oktoba 2017 (Jumanne wiki iliyopita), siku ambayo ilitarajiwa maamuzi mazito ya baadhi ya kesi hizo kutolewa baada ya usikilizaji wake kukamilika. Jaji Dyansobera baada ya kusikia hoja hiyo, akitii muongozo wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kwa suala kama hilo, alielekeza kwamba wenye nia hiyo wawasilishe hoja zao kesho yake – Jumatano.
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.