BAADA YA SERIKALI YA JPM KULIFUNGIA GAZETI LA FREEMAN MBOWE,,SASA MBOWE KUIBUKA KIVINGINE,SOMA HAPO KUJUA - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Tuesday, 14 November 2017

BAADA YA SERIKALI YA JPM KULIFUNGIA GAZETI LA FREEMAN MBOWE,,SASA MBOWE KUIBUKA KIVINGINE,SOMA HAPO KUJUA

IKIWA mwezi mmoja kupita baada ya Serikali ya Rais John Magufuli kulifungia Gazeti la Tanzania Daima kwa siku 90 baada ya kuandika habari zinazodaiwa kuwa zinakiuka kanuni za uandishi wa habari,Wamiliki wa Gazeti hilo wamejipanga kuja kivingine.
 Gazeti la Tanzania  ambalo  linamilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe ,kwa sasa wamejipanga kulirudisha Gazeti la Michezo la Sayari kwa ajili ya kuendelea kuihabarisha jamii.
Taarifa kutoka   ndani Kampuni ya Free Media ambao ni wachapishaji wa Gazeti hilo wamesema Gazeti la Sayari linatarajiwa kutoka wakati wowote kutoka sasa.
“ Kwa sasa Gazeti la Tanzania Daima limefungwa waandishi wetu wanakosa kipato ,wauzaji,wasambazaji pamoja na watu masoko hawana kazi kwahiyo tumeona tulirudishe tena mtaani Gazeti la Sayari ambalo tulilisimamisha kidogo kulichapisha ,”
“Hujue Bwana  hawa majamaa lengo lao ni kumfirisi Mbowe tu kutakana na mambo  ya kisiasa,lakini Mbowe mwenyewe anasema kila Siku Mtu haishi kwa Mkate tu anaishi kwa Neno,kwahiyo hata kama wakimfirisi mali zake wakimfungia magazeti yake lakini atafanikiwa tu kwenye mpango wake kuwakomboa watanzania”Kimesema Chanzo chetu hicho .
Kuja kwa Taaarifa hizi kuna kuja iikiwa ni bado wadau mbali mbali wa Habari wakiituhumu serikali ya Rais Magufuli kwa kuminya uhuru wa habari kwa hatua yake ya kufungia fungia Magazeti huku kwa kipindi cha miaka miwili yamefungiwa magazeti zaidi ya 400 kwa sababu mbali mbali huku mengine yakifutiwa usajili kutokana na kutochapishwa kwa mda mrefu pamoja na mengine yanadaiwa kufungiwa kwa kukiuka kanuni za uandishi 

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.