Urusi:Marekani inatafuta tu kisingizio cha kuivamia Korea Kaskazini - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Friday, 1 December 2017

Urusi:Marekani inatafuta tu kisingizio cha kuivamia Korea Kaskazini

[​IMG]

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov amesema kwamba Marekani imekua ikiichokoza makusudi Korea Kaskazini. Urusi inasema kwamba wanashuku kwamba Marekani inatafuta tu sababu ama kisingizio cha kuivamia Korea Kaskazini. 

Akitoa maelezo kuhusiana na kombora la masafa marefu lilirorushwa na Pyongyang bwana Lavrov amesema kwamba matendo ya hivi karibuni ya Marekani yamelenga wazi kuichokoza Korea kaskazini ili tu ipate sababu ya kuishambulia. 

"Marekani inatakiwa ieleze wazi ni nini hasa wanachokitafuta"

"Iwapo wanataka kuiangamiza Korea Kaskazini kama alivyosema balozi wa Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa"

Lavrov aliendelea kueleza kwamba Pyongyang ilisitisha kufanya majaribio yake ya makombora karibu miezi mitatu lakini ilichokipata toka kwa Marekani ni vitisho ikiwemo kutuma ndege za mashambulizi ya nyuklia na mazoezi mbalimbali ya kijeshi karibu na mipaka yake. 

Bwana Lavrov alieleza kwamba mazungumzo ndio njia pekee ya kutatua mgogoro huo. 

China na Urusi zilipendekeza kusitishwa kwa urushwaji wa makombora toka Pyongyang huku Marekani ikitakiwa kusitisha mazoezi yake ya kijeshi na Korea Kusini(Mpango huo umepewa jina "double freeze").Huku Pyongyang ikionekana kufuata sera hiyo kwa kutojaribu makombora kwa karibu siku sabini lakini mazoezi ya kijeshi kati ya Marekani na Korea kusini yaliendelea ikiwa ni jibu la Marekani kukataa mpango huo wa "double freeze "uliopendekezwa na China na Urusi. 

RT

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.