Mnyika akana uvumi kwamba amejiuzulu - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Tuesday, 5 December 2017

Mnyika akana uvumi kwamba amejiuzulu


 Mbunge wa Kibamba, John Mnyika amesema taarifa kwamba amejiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema -Bara hazina ukweli.
Mnyika ambaye amekuwa akitajwa tajwa kwamba atakihama chama hicho, ametoka kauli hiyo baada ya kuwapo taarifa kwamba  amejiuzulu wadhifa huo.
Akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Desemba 5,2017 jioni kuhusu taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu; Mnyika amesema, ‘’Si kweli ni taarifa za uongo.’’

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.