
Watu wenye silaha wamevamia nyumbani kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha Mhe.Joshua Nassari maeneo ya USA River, usiku wa kuamkia leo na kufyatua risasi kadhaa ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nyumbani hapo.
Nassari na mkewe walifanikiwa kutoroka, kisha kuripoti tukio hilo Polisi. Kamanda wa Polisi Arumeru, amesema wanafanya uchunguzi kubaini watu hao.
Haya ndiyo maneno ya Joshua Nassari kupitia ukurasa wake wa Twitter
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.