
Sentensi nne za Kubenea baada ya kuhusishwa kuhamia CCM
"Kuna watu wasomi wamelitumikia Taifa hili kwa miaka mingi hawajapewa stahili yao , lakini leo hii kuna mtu hana vyeti na anatumia jina la mtu mwingine. halafu mnaniambia nikajiunge na Chama hicho? haiwezekani" S. Kubenea
"Sijawahi kuhongwa, mimi sina bei, bei yangu ni utu wangu.. Hizi zote ni propaganda za CCM ili wasihojiwe mambo ya msingi, wamesema wanatoa milioni 50 kila kijiji ziko wapi?" S. Kubenea
"Mimi sina mpango wowote wa kuondoka Chadema na sijawahi kuzungumza na mtu yeyote kuhama Chadema" S. Kubenea
"Leo hii CCM inarudisha biashara ya utumwa ya kununua watu, Mbunge wa Arumeru Mashariki alipeleka ushahidi TAKUKURU, lakini tunaona Rais alimpandisha cheo mtuhumiwa, siwezi kujiunga na chama hicho hata siku moja"- S. Kubenea.
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.