Chadema Waivaa NEC Kumtaja Mgombea Ubunge Singida Mashariki - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Wednesday, 20 December 2017

Chadema Waivaa NEC Kumtaja Mgombea Ubunge Singida Mashariki



Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) amesikika asubuhi hii wakati akihojiwa na Radio Clouds Fm kwenye kipindi cha Power Breakfast, akisema kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimechukua fomu za kugombea ubunge katika uchaguzi wa marudio Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida. Kupitia taarifa hii ya awali, tungependa vyombo vya habari na umma kwa ujumla ujue kuwa;
1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakijateua mgombea kuwania nafasi ya ubunge katika uchaguzi huo wa marudio, Jimbo la Singida Kaskazini.
2. Mkurugenzi wa NEC, Ndugu Ramadhan Kailima atambue kuwa suala la kugombea nafasi ya ubunge kwa mchakato wa ndani ya CHADEMA linasimamiwa na Kamati Kuu ya Chama na hivyo hivyo yeye hana mamlaka wala hawezi kuwa
msemaji wa suala hilo katika hatua ya sasa.
 3. Tunafuatilia kupata taarifa za kina kuhusu msingi wa kauli ya Mkurugenzi hiyo, kisha tutatoa taarifa kamili katika hatua ya baadae. Imetolewa na Tumaini Makene Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.