SIASA HAINA ADUI WA KUDUMU WALA RAFIKI WA KUDUMU - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Monday, 6 November 2017

SIASA HAINA ADUI WA KUDUMU WALA RAFIKI WA KUDUMU

Image result for MAGUFULI AKISALIMIANA NA LOWASA

SIASA SIO UADUI

Ukweli usiopinga siasa kama siasa haina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu, na usemi umedhihirishwa kupitia watu mbalimbali hapa nchini.

Chama cha Demokrasia na maendeleo chadema kilikuwa kinyume sana na Kada mkubwa wa chadema kwa sasa ambye pia amewahi kuwa kada wa ccm na pia ameitumikia nchi kama waziri mkuu Edward LOwasa , mwaka 2015 akageuka kuwa Rafiki mkubwa wa chadema.Pia kuna baadhi ya viongozi mbalimbali walio kihama chama cha mapinduzi wakati wa kampeni na baadae kurudi na kupewa uongozi mkubwa ( kuna kiongozi alisema Lowasa ni Joshua aliyetumwa na mungu kuwakomboa watanzania ) lakini leo hii ni kiongozi tena mteuliwa wa rais.

Hivi karibuni tumeshuhudia Nyalandu akihama chama cha mapinduzi na kupokelewa na chadema, Nyalandu alipokuwa waziri wa mali asili alikuwa na kashfa nyingi na baadhi ya viongozi wa chadema walimtuhumu kwa kutumia madaraka yake vibaya lakini leo hii amepokelewa kwa mikono miwili.

Nape Nnauye licha kuvuliwa uwaziri wa utamaduni na habari lakini bado anatumaini na mwenyekiti wake wa chama na amedhihirisha hayo kwa kumpongeza kwa kutawala kwa miaka miwili na kutimiza ilani ya chama.
Hapa ndio tunatambua kwamba haina adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu.


Image may contain: 2 people, text

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.