RC Zambi: Watumishi wasiofanya mazoezi kukiona - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Sunday, 12 November 2017

RC Zambi: Watumishi wasiofanya mazoezi kukiona

Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ameonya kuwa watumishi wa umma wasiofanya mazoezi mkoani humo watachukuliwa hatua za kisheria, na kumtaka Katibu Tawala wa mkoa kutekeleza jukumu hilo.

Godfey Zambi ameyasema hayo Jumamosi hii baada ya watumishi wa umma kutohudhuria mazoezi ambayo alikuwa akiyasimamia, na kumtaka Katibu tawala Radhani Katwa kuwachukulia hatua kwani watumishi hao watakuwa wamepuuza agizo la Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, la kutaka wananchi wafanye mazoezi ili kujiepusha na magonjwa.

Zambi amesema kitendo cha watumishi hao kutojitokeza ni kumdharau Makamu wa rais na kutaka kila Jumamosi ya pili ya mwezi watumishi na wananchi wote kujumuika kwa pamoja na kufanya mazoezi, na kuwataka wajitokeze kwa wingi siku ya kufanya usafi ili kutii amri ya Rais na kutunza mazingira.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.