RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP ATEMBELEA TOKYO JAPAN - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Sunday, 5 November 2017

RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP ATEMBELEA TOKYO JAPAN

Rais wa Marekani Donald Trump amewasili mjini Tokyo, Japan, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kama rais, barani Asia.
Mara tu baada ya kuwasili Trump amesema kuwa hakuna kiongozi yeyote wa kiimla au utawala wowote anapaswa kudharau uwezo wa Marekani na kuapa kuwa nchi yake haitalegeza katika kuulinda uhuru wao.
Trump na mke wake, Melania, wanatarajiwa kukutana na wanajeshi wa Marekani walioko nchini Japan.
Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, baada ya kukutana na Mfalme Akihito na Malkia Michiko katika kasri la Imperial.
Ziara ya Trump ni ya kwanza ndefu ya kidiplomasia kufanywa na kiongozi wa Marekani katika miongo kadhaa. Trump atazizuru pia Korea Kusini, China, Vietnam na Ufilipino ajenda kuu ikiwa ni biashara na kukabiliana na mgogoro wa Korea Kaskazini.
Image may contain: 2 people, people standing and suit

Image may contain: 1 person, smiling, standing


Image may contain: 2 people, people smiling, suit

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.