POLISI WAMEKAGUA OFISI YA ACT NA KUKUTA VITU HIVI - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Tuesday, 7 November 2017

POLISI WAMEKAGUA OFISI YA ACT NA KUKUTA VITU HIVI

KWA mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Uenezi, Itikadi na Mawasiliano ya Umma wa ACT-Wazalendo Ado Shaibu amesema  polisi wamekamilisha upekuzi wao katika ofisi za chama na kutoka na vitu vifuatavyo;

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe

1. Taaarifa ya Kamati ya Uongozi kwa Waandishi wa Habari (Press Release) ya Tarehe 21 Oktoba 2017 yenye kichwa cha habari "Kamati Kuu ya ACT Wazalendo Kujadili Hali Mbaya ya Uchumi wa Nchi, Mdororo wa Usalama na Kuminywa kwa Demokrasia"

2. Taarifa ya Kamati Kuu kwa Waandishi wa Habari (Press Release) ya Tarehe 28 Oktoba 2017 yenye kichwa cha habari "Ushahidi Kuhusu Kusinyaa kwa Uchumi wa Nchi Tofauti na Majigambo ya Serikali ya Awamu ya Tano.

3. Vifaa vya Kielektroniki (Laptop na Flash) vilivyotumika kuandaa taarifa hizo.

Hata hivyo polisi walipofika makao makuu ya chama hicho majira ya mchana waligoma Kupekuliwa kwa sababu  Katibu Mkuu hakuwepo ofisini.

Polisi walifika wakakutana na Katibu wa Uenezi, Itikadi na Mawasiliano ya Umma, ndugu Ado Shaibu, ambaye baada ya kuwapokea aliwaeleza kuwa mwenye Ofisi ni Katibu Mkuu ambaye hayuko Ofisini, na kuwa kama Jeshi la Polisi lilitaka kufanya Upekuzi kwenye Ofisi za ACT Wazalendo, nafasi nzuri kwao ilikuwa ni jana kwa kuwa walimhoji Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo kwa Masaa 7.

Lakini Polisi walisisitiza kufanya upekuzi leo, hivyo wakaamua kumfuata Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu, nyumbani kwake ili awepo wakati wa upekuzi husika

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.