MKE WA MUGABE, GRACE MUGABE AMUOMBA MUME WAKE KUPOKEA NAFASI YA KUTAWALA ZIMBABWE
Mke wa Robert Mugabe(Grace Mugabe) amesema yupo tayari
kupokea kijiti cha Urais kutoka kwa Mume wake na amemuomba mume wake kumruhusu
kuchukua nafsi hiyo. Zimbabwe wanatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwaka 2018 ,watu
wengi nchini Zimbabwe wamekuwa wakijiuliza nani atapokea kijiti cha Uraisi
kutoka kwa Kiongozi Wa sasa Robert
Mugabe ambaye Umri umeenda na hana vigezo vya kugombea tena, Hivi karibuni
Amnesty international walitoa taarifa kwamba Robert
Mugabe na mpinzani wake Mkubwa nchini humo Morgan Tsvangirai hawana sifa za kugombea tena na hii ni kutokana
na umri wao kuwa mkubwa sana Robert mugabe ana umri wa miaka 93.
Grace Mugabe amesema haogopi kuchukua nafasi hiyo , akasema
kama mume wake anataka kumpa kazi ampe bure yeye haogopi “ mimi siogogopi kama unataka
kunipa nipe tu usiwe na wasiwasi na mimi”
Taarifa zinasema makamu wa raisi wa nchi alitegemewa kupokea kijiti cha Uraisi kutoka kwa Rais Mugabe mwenye umri wa
miaka 93 lakini kwa sasa Makamu wa raisi hana mahusiano mazuri na Rais Mugabe
na siku za karibuni Mugabe Alitangaza kumfukuza makamu kwa kufanya njama za kutafuta watu wa
kumsaidia katika uchaguzi mkuu ujao.
Chama kipo kwenye mpasuko
kwa sababu hawajui nani atakuwa Rais , GRACE MUGABE pia alisema hivi
karibuni watabadilisha katiba ili iweze kuwaruhusu wanawake kuwa makamu wa rais.
Grace Mugabe anasema makamu wa Rais wa sasa alipanga njama
mwaka 2014 za kuipindua serikali.

No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.