MHASIBU AKAMATWA OFISINI USIKU AKIPORA - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Thursday, 23 November 2017

MHASIBU AKAMATWA OFISINI USIKU AKIPORA



Aliyewahi kuwa mhasibu wa hospitali ya mkoa wa Singida na baadae kuachishwa kazi kwa sakata la vyeti feki anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukutwa ndani ya ofisi aliyokuwa akifanyia kazi majira ya saa sita usiku akiwa na zaidi ya shilingi laki nane alizoiba ndani ya ofisi hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Debora Magiligimba amesema Edith Talasi amekamatwa usiku huo akiwa amejifungia ndani ya ofisi ya uhasibu ya hospitali hiyo baada ya jeshi la polisi kupewa taarifa ya kuwepo kwake hapo.
Inadaiwa kuwa aliingia ofisini humo kwa kutumia funguo za ziada bandia alizokuwa nazo.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.