KENYATA ATASUBIRI SIKU 14 KUAPISHWA - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Tuesday, 7 November 2017

KENYATA ATASUBIRI SIKU 14 KUAPISHWA


Image may contain: 1 person
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya atasubiri kwa siku 14 zaidi kabla ya kuapishwa baada ya kesi mbili kupelekwa katika mahakama ya juu zikipinga ushindi wake katika uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26.
Harun Mwau, mwanasiasa aliyekuwa mjumbe wa Kilome ni baadhi ya waliopeleka kesi mahakamani wakipinga ushindi wa Rais Uhuru. Katika kesi yake, Mwau anadai kuwa uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26 ulifanywa kinyume na sheria. Mwau anadai kuwa tume ya uchaguzi wa kitaifa (IEBC) ilikiuka katiba kwa kuandaa uchaguzi huo bila kuagiza vyama husika kufanya upya mchujo wa wagombea kama inavyoagiza katiba. Wakati huo huo mashirika mawili ya kiraia pia yamefikisha kesi mahakamani yakipinga uhalali wa uchaguzi huo. Miongoni mwa mashtaka mengine, mashirika hayo yanadai kuwa IEBC iliongeza majina zaidi katika orodha ya wagombea kinyume na sheria.
Majaji wa mahakama ya juu sasa wako na siku 14 kuamua iwapo uchaguzi huo ulikuwa halali au la. Iwapo mahakama itafutilia mbali uchaguzi huo basi itaagiza uchaguzi mwingine kufanywa katika muda wa siku 60. Mahakama hiyo ilifuta uchaguzi wa Agosti 8 ambao Rais Uhuru alitajwa kushinda na kuagiza kuandaliwa kwa uchaguzi mwingine katika kipindi cha siku 60. Uchaguzi huo wa marudio uliendelea Oktoba 26 licha ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kujiondoa na wafuasi wake kususia.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.