
SIKU chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kujivua uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na nafasi yake ya ubunge na kujiunga na Chadema, ameanza kuonja chungu ya uamuzi wake, baada kushutumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka,
Shutuma hizo dhidi ya Nyalandu zimeibuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla bungeni leo alipokuwa akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018.
Dk Kigwangalla ameiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu kwa matumizi mabaya ya madaraka ili sheria ichukue mkondo wake.
Waziri huyo amesema Nyalandu alipokuwa waziri aliikosesha serikali mapato ya Sh. 32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.
Taarifa hiyo ya Kigwangalla inakuja ikiwa kuna Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Serikali ambazo Fullhabari.blog imezipata zinasema iwe isiwe lazima Nyalandu ambaye aliwai kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM katika uchaguzi wa mwaka 2015 afikishwe mahakamani.
"Sikifichi bwana Nyalandu lazima afikishwe Mahakamani ,watu wameshandaa ya kuandaa wewe utaamini tu,"Kimesema Chanzo chetu hicho.
Mbali na Chanzo hicho,nao Kauli hiyo ya Kingwangalla inatajwa na Wachambuzi wa siasa kuwa ni ya kisasi tu kwa Nyalandu ambaye ni Mwanasiasa kijana mwenye mvuto nchini.
Mbali na Chanzo hicho,nao Kauli hiyo ya Kingwangalla inatajwa na Wachambuzi wa siasa kuwa ni ya kisasi tu kwa Nyalandu ambaye ni Mwanasiasa kijana mwenye mvuto nchini.
Wachambuzi hao wamesema kinachomkuta Nyalandu kishamkuta Aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tanu,Freedrick Sumaye ambaye alipohamia chadema yakamkuta.
"Ujue sasa hapa ni kisasi tu,haiwezekani hawa watu wakiwa CCM haguswi kabisa ila mtu akihama chama tu zinaibuka kashfa lukiki,hawezekani na hatuwezi kujenga nchi hivi"
"leo Sumaye kahamia Chadema tumeona Mashamba yamechukuliwa,leo lowassa kahamia Chadema tumeonaRedio Five ambayo ni ya kwake imefungiwa sasa tunakwenda wapi"alihoji Mchambuzi wa Masuala ya siasa kutoa Chuo Kikuu huria nchini ambaye aliomba jina lake litajwe mtandaoni
Mbali na tuhuma hiyo, pia alimtuhumu kutumia helkopta ya mwekezaji mmoja raia wa kigeni, kipindi cha kampeni zake za kugombea urais 2015, wakati kampuni ya raia huyo ilikuwa ikituhumiwa kwa ujangili.
Nyalandu aliwahi kuliliwa akisema kuwa tuhuma ambazo zimeanza kuibuliwa mitandao dhidi yake si za kweli bali zinalenga tu kumchafua na kuhoji iweje ziibuliwe sasa zaidi ya miaka miwili tangu aachie uwaziri
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.