Aliyedai Acacia Haina Hela Ya Kulipa Serikali ‘Abwaga Manyanga’ - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Thursday, 2 November 2017

Aliyedai Acacia Haina Hela Ya Kulipa Serikali ‘Abwaga Manyanga’



Ofisa Mtendaji Mkuu na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya Madini ya Acacia wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao rasmi kuanzia leo, Alhamisi, Novemba 2, 2017. Vigogo hao katika Kampuni hiyo inayosubiriwa kutekeleza makubaliano baina yake na Serikali wametoa sababu za maamuzi hayo kupitia barua walizoandika ambapo, Ofisa Mtendaji Mkuu, Brad Gordon amesema kuwa anataka kurudi nyumbani kwao Australia kusimamia masuala ya kifamilia huku Ofisa Mkuu wa Fedha, Andrew Wray akisema kuwa amepata fursa nzuri zaidi sehemu nyingine. 11/3/2017 Aliyedai Acacia Haina Hela Ya Kulipa Serikali ‘abwaga Manyanga’ -manyanga 2/10 Hatahivyo, licha ya kutangaza uamuzi huo leo, wawili hao wataendelea kuhudumu kwenye nafasi hizo wakati wakikabidhi majukumu ya kiofisi kwa warithi wao. Kuziba mapengo hayo, Bodi ya Wakurugenzi ya Acacia imemtangaza Peter Geleta kuchukua nafasi ya Ofisa Mkuu Mtendaji huku Jaco Maritz akitangazwa kusimamia masuala yote ya fedha ya kampuni hiyo. Hivi karibuni Serikali na Kampuni ya Barrick Gold Mine inayomiliki asilimia 63.9 ya hisa za Acacia waliafikia makubaliano katika masuala kadhaa baada ya majadiliano yaliyochukua muda wa miezi mitatu ambapo kampuni hiyo ilikubali kutekeleza masharti yote katika sheria mpya ya madini ikiwa ni pamoja na kulipa Dola milioni 300 za Marekani huku majadiliano zaidi kuhusu kodi yakiendelea. Siku moja baada ya kutangazwa kwa makubaliano hayo, Ofisa Mkuu huyo wa Fedha, Wray alinukuliwa akiwaambia wanahabari kuwa Acacia haina uwezo wa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa wakati mmoja.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.