Tundu Lissu: Ameongea na Watanzania kuhusu mambo kadhaa. - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Tuesday, 31 October 2017

Tundu Lissu: Ameongea na Watanzania kuhusu mambo kadhaa.


Ameanza kwa kumshukuru Lazaro Nyalandu kwa Kuikimbia CCM na kuomba kujiunga CHADEMA. "Lazaro Nyalandu bado ana Mawazo ya Ujana".

Kingine alichozungumzia ni Uchaguzi mdogo wa Madiwani wa kata 43. Amesema watu wasiichague CCM. Amesema kuichagua CCM ni sawa na kukubali CCM wawndelee kufanya wanayoyafanya, nawaomba mfanye maamuzi Magumu.

Tukatae Mateso, tukatae Utawala wa Bomoabomoa, tukatae utawala wa kuokota maiti baharini kama samaki, tukatae utawala wa Kamatakamata, tuikatae CCM.

Nlipigwa risasi na walewale waliomfunga Diwani wa kata wa Siuyu bwana Gerald.

Walinifungulia mashitaka mara nyingi na waliposhindwa kunifunga wakaamua kunipiga risasi lakini Mungu kaniponya.

Kawaasa Wananchi wa Kata ya Siuyu Singida kuonyesha hisia zao. Amesema Watesi wetu wamelazimisha leo niongelsw kitandani badala ya kuja kuongelea huko.

Kwenye huu Uchaguzi Mdogo tuwape Fundisho watesi wetu.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.