MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kumatwa kwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini. Anaripoti Faki Sosi… (endelea).
Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri leo tarehe 8 Novemba mwaka 2018 ameamuru kukamatwa kwa viongozi hao kutokana na kushindwa kuhudhuria kwenye kesi inayowakabili hapo bila ruhusa ya mahakama.
Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinaeleza kuwa, Mbowe amwekenda nchini Afrika Kusini kwa matibabu. Pia mahakamani hapo mdhamini wa kiongozi huyu ameeleza kuwa, yupo nje ya nchi kwa matibabu.
Mdhamini wa Matiko ameieleza mahakama kuwa, mshtakiwa amepata ziara ya kibunge na yuko nchini Burundi pamoja na kuwasilisha vielelezo ikiwamo tiketi ya ndege.
Kesi inayowakabili Mbowe na viongozi wengine waandamizi ni kufanya maandamano yasiyokuwa ni kufanya maandamano bila kibali.
Viongozi wengine kwenye kesi hiyo ni pamoja na Dk. Vicent Mashinji Katibu Mkuu wa Chama Hicho ,Peter Msigwa Mbunge Iringa Mjini, Halima Mdee, Mbunge wa Kawe John Mnyika (Mbunge Kibamba)).
Wengine ni Salum Mwalimu Naibu Katibu wa Chama hicho Zanzibar , John Heche Mbunge wa Tarime Vijijini. na Easter Bulaya (Mbunge Bunda.
Wakati huo huo Wakili Jamhuri Johnson, anayemtetea Mchungaji Peter Msigwa, katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, ametangaza kujiondoa kumtetea kwa madai ya kutorishishwa na mwenendo wa kesi hiyo unavyoendeshwa.
Wakili Johnson amedai kuwa, mwenendo wa kesi hiyo hauridhishi na kwamba hajawahi kukutana na kesi ya namna hiyo kwa miaka 20 ya uwakili wake.
Watuhumiwa wote wamegoma kujibu chochote wakati walipokuwa wakisomewa maelezo ya awali kwa madai hawawezi kueleza chochote kutokana na kutokuwa na wakili wa kuwatetea.
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.