Dar es Salaam. Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekitoza faini ya Sh7.5 milioni kituo cha televisheni cha Star kwa kukiuka kanuni za utangazaji.
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Joseph Mapunda amesema kituo hicho kilitangaza habari ambazo hazikuthibitishwa za uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika Novemba 2017.
Amesema kituo hicho kilitangaza habari kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuwa kwenye uchaguzi huo watu walipigwa bila uthibitisho kutoka Polisi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mapunda leo Jumanne Januari 2,2018 amesema jijini Dar es Salaam kuwa, kituo hicho kinatakiwa kulipa faini hiyo katika kipindi cha siku 30 kuanzia leo.
Amesema kituo hicho pia kitakuwa katika uangalizi wa TCRA.
Mamlaka hiyo pia imekitoza faini ya Sh7.5 milioni kituo cha televisheni cha Azam Two kwa kutangaza uchochezi.
Kituo hicho kimetozwa faini kwa kutangaza taarifa za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Novemba 2007 bila kupata upande wa pili wa NEC na Polisi.
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.