KUFUNGIA MAGAZETI MENGI,,MTATIRO AIBUKA NA KUICHANA SERIKALI,SOMA HAPO KUJUA - Siasa News

Breaking

Siasa ni Maisha

Monday, 11 December 2017

KUFUNGIA MAGAZETI MENGI,,MTATIRO AIBUKA NA KUICHANA SERIKALI,SOMA HAPO KUJUA


NA KAROLI VINSENT
WAKATI Serikali ya Rais John Magufuli ikitajwa kuwa ni serikali pekee iliyofungia Magazeti mengi kwa kipindi kifupi,Hatua hiyo imewaibua vyama vya Upinzani nchini baada ya kusema serikali inarudisha nchi kwenye zama za ukoroni.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar Es Salaam,na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi CUF ,Julias Mtatiro wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema   kwa kipindi kifupi cha Miaka miwili serikali ya Rais Magufuli  kuyafungia Magazeti ya Mwanahalisi,Mseto,Mawio,Raia Mwema,Tanzania Daima kwa madai kuwa yanaandika habari za Uchozezi .
Amesema hatua hiyo ni ya kuminya uhuru wa kujieleza na yanarudisha nchi  kwenye kipindi cha Ukoroni.
"Leo unafungia Gazeti kisa limetoa takwimu za uongo ,,huu ni uonevu Gazeti umelifungia limetoa ajira kwa watu zaidi hamsini leo hawana kazi,,harafu wewe unasema unakuza uchumi uchumi gan?"
"Gazeti kama limekosea kutoa takwimu linaweza kuomba radhi na sio kulifungia ,leo tunarudisha nchi kwenye zama za ukoroni " Mtatiro.

Kauli hiyo inakuja huku ikiwa bado sekta ya habari ikiwa kwenye wingu zito baada ya vyombo vya habari na waandishi wa habari wakiwa kwenye uoga wa kuandika habari za kuikosoa serikali kwa kile kinachoelezwa kuogopa vyombo vyao kufungiwa.

Uoga huo umekifanya kituo cha Sheria na Haki za Binadamu /LHRC/  kukiri kwa sasa mazingira ya wanahabari nchi ni magumu kutokana na wanahabari kujaa uoga.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.