Nyalandu Ajivua uwanachama wa CCM pia amejivua na Ubunge.
Anaonge Lazaro Nyalandu;
“Rasmi; Kujiuzuru yangu Nafasi ya ujumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM pamoja na nafasi zote ndani ya chama cha mapinduzi kuanzi aleo Oktoba 30 mwaka 2017”
Anaonge Lazaro Nyalandu;
“Rasmi; Kujiuzuru yangu Nafasi ya ujumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM pamoja na nafasi zote ndani ya chama cha mapinduzi kuanzi aleo Oktoba 30 mwaka 2017”
Halikadhalika asubuhi ya leo nimemuandikia Mhe. spika wa Bunge Job Ndugai, barua ya kujiuzulu rasmi nafasi yangu ya ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini kupitia CCM, nafasi ambayo nimeitumika kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa mara ya kwanza mwaka 2000 hadi sasa
Aidha nimechukua uamuzi huo kutokana na kutokulidhishwa kwangu na muenendo wa hali ya kisiasa nchini ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa watanzania wenzangu na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi ya mihimili ya dola yaani Serikali, Bunge na Mahakama. Tunapofanya utendaji wa kazi wa kutunga sheria na kusimamia kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana kikatiba.
Vile vile naamini bila Tanzania kupata katiba Mpya sasa hakuna namna yoyote ya kufanya mihimili ya dola isingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na Mahakama ambayo ndio chimbuko na uongozi bora la nchi na kuonyesha kwa wazi kuwa madaraka yote yanatokana na wananchi wenyewe na kwamba serikali ni sharti iwe ya watu kwa ajili ya watu
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.